Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

UISLAMU NA IMANI

 

1. Imepokewa kutoka kwa Sufyan bin Abdallah (R.A.A.) kuwa alisema, nilisema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nambie neno moja tu ya kunitosheleza kuhusu uislamu kwa jumla, neno ambalo baada yake sitamuuliza ye yote”. Mtume (S.A.W) akamjibu, “Sema nimemuamini Allah (S.W.T) kuwa ni mola wangu wa pekee, kisha nenda mwendo uliyonyooka”. (Muslim)

2. Imepokewa kutoka kwa Anas (R.A.A) kuwa mtu mmoja katika waarabu wa majabalini alimuuliza Mtume (S.A.W), “kiyama ni lini?” Mtume (S.A.W) akamjibu kumuuliza “Umejiandalia nini?” Mtu huyu akasema, “Mapenzi ya Mungu na Mtume wake”. Mtume (S.A.W) akamwambia, “Basi wewe utakuwa pamoja na unaowapenda”. (Bukhari na Muslim)

3. Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Umar (R.A.A) kuwa alisema, Mtume (S.A.W) amesema, “Uislamu umezelekwa msingi wake (umejengwa) juu ya nguzo tano, (1) kuweka wazi na kukubali kabisa kwamba hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba hapana shaka Muhammad (S.A.W) ni Mtume wake, (2) kuimarisha swala, (3) Kutoa Zaka, (4) kukusudia nyumba tukufu (kuenda Hijja), (5) kufunga mwezi wa Ramadhan. (Bukhari na Muslim)

4. Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Amri bin Al-Aas (R.A.A) kuwa Mtume (S.A.W) amesema, “Madhambi makubwa zaidi ni kumshirikisha Mungu, kutowatii wazazi wawili, na kuiua nafsi, na kula kiapo cha urongo”. (Bukhari)

5. Imepokewa kutoko kwa Abu Hurairah (R.A.A.) kuwa alisema, Mtume (S.A.W) amesema, “Muislamu aliyekamilika kiimani ni yule aliye na tabia bora kuliko wenzake, na wabora wenu ni wale walio mabora kwa wake zao” (kwa tabia mzuri). (Tirmidhi)

6. Imepokewa kutoka kwa Anas (R.A.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) amesema, “Mmoja wenu hawi Muislamu (Muumini aliyekamilika) ila atakapompendelea ndugu yake kile anachojipendelea yeye mwenyewe”. (Bukhari na Muslim)

7. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.A) kuwa Mtume (S.A.W.) alisema, “Naapa kwa Mola wangu, haijakamilika imani yake; Naapa Kwa Mola wangu, haijakamilika imani yake; Naapa kwa mola wangu, haijakamilika imani yake!” Akaulizwa Mtume (S.A.W), “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani huyo?” Mtume (S.A.W) akasema, “Ni yule ambaye jirani yake hakusalimika na vitimbi vyake”. (Bukhari na Muslim)

8. Imepolewa kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.A) kuwa Mtume (S.A.W) amesema, “mara nyingi mtu hufuata dini ya rafiki yake mpendwa, kwa hivyo mtu atazame ni nani wa kuwa rafiki yake”. (Abu Dawud na Tirmidhi)

 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS