WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
UNYENYEKEVU KWA WAZAZI NA JAMAA
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Pua yake ishike vumbi, Pua yake ishike vumbi, Pua yake ishike vumbi (maana kudhalilika) aliyewakuta wazazi wake wawili katika uzee au mmoja wao, pamoja na hivyo akawa hataingia peponi” (kwa kutowatendea mema). (Muslim)
2. Imepokewa kutoka kwa Abu Muhammad Jubair bin Mut‘im (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema “Hatoingia peponi anayekataa ukoo wake” (au kizazi chake). (Bukhari na Muslim)
3. Imepokewa kutoka kwa Anas (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Anayependa akunjuliwe riziki yake na umri wake urefushwe basi aunge kizazi chake” (Awatendee wema wale wanaozalikana na yeye). (Bukhari na Muslim)
4. Imepokewa kutoka kwa Baraa Bin Aazib (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Khalati (mama mdogo) yuko katika daraja ya mama mzazi”. (Tirmidhi)
5. Imepokewa kutoka kwa Bin Umar (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Hakika ya wema bora zaidi ni mtu kuwatendea mema marafiki wa babake”. (Muslim)