Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

MWENENDO MZURI

 

1.  Imepokewa kutoka kwa Abu Darda (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Hakuna kitu kilicho na uzito sana katika mizani ya Muislamu siku ya kiyama kuliko tabia nzuri, na hakika Mwenyezi Mungu humchukia mtu mbaya mwenye kuropoka na maneno machafu”. (Tirmidhi)

2.  Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa kuna mtu alitaka wasia kutoka kwa Mtume (ص ). Mtume (ص ) akamwambia “Usitawaliwe na hasira”. Yule mtu akalirudia ombi lake mara kadha wa kadha, na kila mara Mtume (ص ) alikuwa akimjibu “Usitawaliwe na hasira”. (Bukhari)

3.  Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) aliniambia mimi  “Usidharau kabisa chochote kile hata kama ni kidogo katika mema na hata ikiwa ni kumkabili ndugu yako kwa uso wenye furaha”. (Muslim)

4.  Imepokewa kutoka kwa Sa‘d Bin Abi Waqqas (ر ) kuwa alisema, “Nilimsikia Mtume (ص ) akisema, “Mungu humpenda mja mchaji Mungu, mkwasi na asiyejitapa”. (Muslim)

5.  Imepokewa kutoka kwa Iyadh Bin Himar (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema “Mungu amenijuza kwa wahyi kuwa mfanye unyenyekevu hata mmoja wenu asipate kujigamba mbele ya mwengine na hata mmoja wenu asimdhulumu mwengine”. (Muslim)

6.  Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Mmoja wenu akialikwa chakula, basi auitikie ualishi. Ikiwa amefunga (saumu) amuombee Mungu mwenyeji wake, na akiwa hakufunga basi na ale”. (Muslim)

7.  Imepokewa kutoka kwa Nawwas Bin Sam‘an (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Wema ni kuwa na tabia nzuri, na ovu (dhambi) ni kilichofuma ndani ya moyo wako (kinachokera nafsi yako), na ukawa hupendi watu wakijue”. (Muslim)

 

 

 

 


 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS