WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
TABIA YA KULA NA KUNYWA
1. Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (ر ) akisema, “Mtume (ص ) alikuwa akiutumia mkono wa kulia katika mambo ya usafi na kwa kulia chakula, na mkono wake wa kushoto msalani na kwa chochote kichafu”. (Abu Dawud)
2. Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (ر ) kuwa alisema, “Mtume (ص ) hakuwahi kabisa kutia ila chakula, akikipenda chakula, hukila na akikichukia hukiacha” (bila kutoa kasoro). (Bukhari na Muslim)
3. Imepokewa kutoka kwa Anas Bin Malik (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema. “Hakika, Mwenyezi Mungu huridhika na mja wake ambaye anapokula chakula humhimidi na kumshukuru juu ya chakula kile na anapokunywa kinywaji humhimidi na kumshukuru juu ya kinywaji kile”. (Muslim)
4. Imepokewa kutoka kwa Abu Qatadah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Mnyweshaji wenzake maji, awe ni wa mwisho kuyanywa”. (Tirmidhi)