WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
DESTURI YA KUSALIMIA
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Sudayy bin ‘Ajlan al-Bahili (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Mtu anayestahiki sana kuwa karibu na Mungu, ni anaye anza kuwasalimia wenzake”. (Abu Dawud)
2. Imepokewa kutoka kwa ‘Abdallah Bin ‘Amr Bin Al-‘Aas (ر ) kuwa mtu alimuuliza Mtume (ص ). “Ni Uislamu upi ulio bora?” Mtume (ص ) akajibu “kuwalisha watu na kumsalimia unayemjua na usiyemjua” (kwa maamkuzi ya Assalamu ‘Alaykum). (Bukhari na Muslim)
3. Imepokewa kutoka kwa Baraa’ (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema, “Waislamu wawili hawakutani na kupeana mikono ila husamehewa madhambi yao kabla hawajatengana’. (Abu Dawud)
4. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Aliyepanda (farasi, punda au gari, baiskeli) yatakikana amsalimie anayetembea, na anayetembea ndie wakumsalimia aliyeketi, na wachache ndio wa kuwasalimia wengi”. (Bukhari na Muslim)
5. Imepokewa kutoka kwa Bi ‘Aisha (ر ) kuwa alisema, “Mtume (ص ) aliniambia, “Huyu ni Jibril anakusalimia kwa maamkuzi ya amani (yaani Assalamu ‘Alaykum)”. Akaendelea Bi ‘Aisha (ر ) kusema ‘Nikamjibu (Jibrili, wa ‘Alayhi salamu wa Rahmatullahi wa Barakatuhu’ (Huku nikusema, Imshukie yeye amani, huruma ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake). (Bukhari na Muslim)
6. Imepokewa kutoka kwa Bin ‘Abbas (ر ) kuwa Mtume (ص ) alipita makaburini katika mji wa Madina, akawalekea kwa uso wake waliokufa huku akisema “Amani iwe juu yenu enyi watu wa makaburi. Mungu atatusamehe sisi na nyinyi. Nyinyi mmetutangulia na sisi tutawafuata”. (Tirmidhi)