WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
REHEMA NA UPOLE
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema, “Mungu alipoumba viumbe aliandika katika kitabu ambacho kiko kwake juu ya kiti chake cha enzi, kuwa huruma yangu inashinda hasira yangu”. (Bukhari na Muslim)
2. Imepokewa kutoka kwa Jarir Bin Abdallah (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema “Asiyewahurumia wenzake basi Mwenyezi Mungu naye hamhurumii”. (Bukhari na Muslim)
3. Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema, “Hakika Mwenyezi Mungu ni mpole na mwenye huruma, na anapenda upole na huruma. Na Mwenyezi Mungu humpa mtu kwa upole mambo ambayo hampi kwa kutumia nguvu, na Mwenyezi Mungu hampi mtu isipokuwa kwa upole.” (Muslim)
4. Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas (ر ) kuwa Mtume (ص ) alimwambia Ashajj Abdilqais (ر ), “Una tabia (sifa) mbili ambazo Mungu anazipenda sana, nazo ni upole na uvumilivu”. (Muslim)