WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
UMUHINU WA KAZI
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Mungu hakumtuma Mtume ye yote ila huyo nabii alikuwa ni mchungaji kondoo”. Kisha masahaba zake wakamuuliza, “Na wewe pia?” Akasema, “Ndio, nilikuwa nikiwachungia watu wa Makkah kwa malipo ya baadhi ya Qirat”. (Bukhari)
(Qirat = kipimo ambacho kadiri yake imebadilika kulingana na zama. Kwa siku hizi ni kiasi cha gramu 1.944 ya dhahabu).
2. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Mtume Daud (Amani iwe juu yake) alikuwa hali kitu chochote ila alichokichuma kutokana na kazi ya mkono wake”. (Bukhari)
3. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema, “Ni bora sana ikiwa mmoja wenu atabeba mzigo la kuni mgongoni kuliko kumuomba mtu, ima ampe au amnyime”. (Bukhari na Muslim)
4. Imepokewa kutoka kwa Bin Umar (ر ) kuwa Mtume (ص ) alisema akiwa juu ya mimbari akizungumza juu ya sadaka na kuto omba omba akasema, “Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, na mkono wa juu ndio unaotoa na mkono wa chini ndio unao omba omba”. (Bukhari na Muslim)