WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
UKARIMU
Imepokewa kutoka kwa Bin Masoud (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Ni watu aina mbili tu ambao wapaswa kuonewa wivu. Wa kwanza ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amempa mali na kisha akampa hidaya ya kutumia mali hiyo kwa njia nzuri na wa pili ni yule ambaye Mwenyezi Mungu amempa hekima na kisha akatumia hekima hiyo katika kutoa hukumu iliyo sawa na pia kuwafundisha hiyo wengine”. (Bukhari na Muslim)
- Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Ukwasi (utajiri) si utajiri wa mali mengi bali utajiri ni utajiri wa nafsi” (utajiri wa moyo). (Bukhari na Muslim)