Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

 

1.   Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Amri bin Al-Aas (R.A.A) kuwa alisema, nilimsikia Mtume (S.A.W) akisema, “Mtu ambaye anani swalia mimi swala mojo (1), basi Mwenyezi Mungu anamswalia yeye kwa sababu ya hiyo swala moja, swala   kumi (10)”. (Muslim)

(sisi Kumswalia Mtume nikumwombeya huruma na baraka za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu kutuswalia sisi ni kutupa baraka zake.)

2.   Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Shikhir (R.A.A) kuwa alisema, “Nilimwendea Mtume (S.A.W) na yeye akiswali, nilisikia mgoromo ukitoka kutoka kifua chake ukiwa kama mlio wa chungu kinachochemka, (Na mgoromo huu) ulikuwa ni kilio chake”. (Abu-Dawud na Tirmidhi)

3.   Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (R.A.A) kuwa alisema, “Mtume aliwakataza maswahaba wake kufunga (saumu) ya kuunganisha mchana na usiku pasina kupumzika, kwa ajili ya kuwahurumia. Kisha maswahaba walimwuliza lakini wewe mbona waunganisha mchana na usiku? Akajibu Mtume (S.A.W) “Mimi si kama nyinyi. Mola wangu hunilisha na kuninywesha usiku”. (anipa nguvu kama aliyekula)        (Bukhari na Muslim)                              

4.   Imepokewa kutoka kwa Anas (R.A.A) kuwa alisema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alikuwa bora wa watu kwa tabia nzuri”. (Bukhari na Muslim)

5.   Imepokewa kutoka kwa Jabir (R.A.A) kuwa alisema, “Mtume hakuwahi kabisa kuombwa kitu kisha akasema la” (kila anpoombwa hutoa). (Bukhari na Muslim)

6.   Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (R.A.A) kuwa alisema, “Maneno ya Mtume (S.A.W) yalikuwa wazi; hufahamika na ye yote anaeyasikia”. (Abu Dawud)

7.   Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (R.A.A) kuwa alisema, “Sikuwahi kumuona Mtume (S.A.W) akifurahika akawa akicheka mpaka magego yake yakaonekana, bali alikuwa akitabasamu.” (Akifunua meno kwa furaha). (Bukhari na Muslim)

8.   Imepokewa kutoka kwa Bin Umar (R.A.A) kuwa Abu-Bakr Siddiq (R.A.A) amesema, “Mtukuzeni Mtume Muhammad (S.A.W) kwa kutukuza jamii yake”.    (Bukhari)


 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS