Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

WAKE WEMA

  1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Mwanamke huolewa kwa mambo manne, kwa mali yake, kwa ukoo wake, kwa urembo wake na kwa mapenzi yake ya dini, jishindie kwa kumpata aliyeshika dini, mikono yako itabarikiwa” (utapata mafanikio mema). (Bukhari na Muslim)
  1. Imepokewa kutoka kwa Abdallah Bin Amr Bin Al-Aas (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Dunia nzima ni pambo jema, na pambo jema zaidi la dunia ni mwanamke mwema” (mke mwaminifu). (Muslim)
  1. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa Ash’ari (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Uvaaji wa nguo za hariri, na dhahabu umeharamishwa kwa umma wangu wa kiume na umehalalishwa kwa umma wangu wa kike”. (Tirmidhi)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS