Imepokewa kutoka kwa Abu Masoud Uqbah Bin Amri Al-Ansari Al-Badri (ر) kuwa alisema, Mtume (ص) amesema “Anayemshiria mwenzake kufanya njema basi naye ana fungu (faida) mfano wa fungu (faida) la mtendaji wa jema hilo”. (Muslim)
Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (ر) kuwa alisema “Nilimsikia Mtume (ص) akisema”, “Ye yote miongoni mwenu atakaye ona ovu basi alikataze na kulipinga kwa mkono wake, asipoweza (au asipofaulu) basi alikataze kwa ulimi wake (kwa kusema) na asipoweza basi alichukie moyoni mwake, na hiyo (ya tatu) ni Imani ya daraja ya chini sana.” (Muslim)