WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa al-Ash‘ari (ر) kuwa alisema, Mtume (ص) amesema “Muislamu na Muislamu mwenzake ni kama matofali ya jengo, hutiliana nguvu zenyewe kwa zenyewe”. Akafanya mfumo kwa vidole vyake vya mikono miwili’ (akionyesha mfano wa watu kuwa kitu kimoja). (Bukhari na Muslim)2. Imepokewa kutoka kwa Nu‘man ibn Bashir (ر) kuwa alisema, Mtume (ص) amesema “Mfano wa Waislamu katika kupendana na kuhurumiana na kusikitikiana kwao ni mfano wa kiwiliwili kizima, kikiteseka kiungo kimoja basi mwili mzima husikia maumivu, kwa kukesha na homa”. (Bukhari na Muslim)