WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah ( ر ) kuwa alisema, Mtume ( ص ) amesema, “Mtazameni aliye katika hali ya chini kuliko nyinyi na wala msimtazame aliyewashinda kwa hali, na kufanya hivyo hamtopata kuidharau neema ya Mungu aliyewapa.” (Bukhari na Muslim)
2. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah ( ر ) kuwa alisema, Mtume ( ص ) alikuwa akimuomba Mungu akimwambia, “Ewe Mwenyezi Mungu, wape watu wa ukoo wa Muhammad kadiri ya mahitaji yao tu.” (Bukhari na Muslim)
3. Imepokewa kutoka kwa Anas Bin Malik ( ر ) kuwa alisema, “Mtume ( ص ) hakuwahi kabisa kula chakula mezani hadi kufa kwake, na wala kula mkate wa unga uliosagwa vizuri na kuchungwa, hadi kufa kwake.” (Bukhari)
4. Imepokewa kutoka kwa Abu Musa al-Ash‘ari ( ر ) kuwa amesema, “Bi Aisha ( ر ) alitutolea na kutuonesha shuka na kikoi kigumu. Kisha akasema, “Mtume ( ص ) alifia katika nguo hizi mbili.” (Bukhari na Muslim)