Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

 

Akhera

 
       1. Imepokewa kutoka kwa Jabir (ر) kuwa alisema, Mtume (ص) amesema: “Kila mtu atafufuliwa katika hali aliyofilia” (yaani mwema kwa wema, na mwovu kwa uovu). (Muslim)

      2.Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر) kuwa Mtume (ص) amesema, “Mja hamsitiri mja mwenzake kutokana na aibu hapa duniani ila yeye pia atasitiriwa na Mwenyezi Mungu siku ya kiyama.” (Muslim)

       

      3.Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر) kuwa Mtume (ص) alisema, “Itawajia siku ambayo mtakuwa na pupa sana ya mamlaka na vyeo, na vitakuwa hivyo vyeo (vikitumiwa vibaya) basi itakuwa majuto siku ya kiyama.” (Bukhari)

       

      4.Imepokewa kutoka kwa Anas (ر) kuwa Mtume (ص) amesema, “Ewe Mwenyezi Mungu hapana maisha bora (halisi) isipokua ni maisha ya akhera.” (Bukhari na Muslim)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS