WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
SWALAH
1. Imepokewa kutoka kwa Abu-Abdul Rahman Abdallah bin Masoud (R.A.A) kuwa alisema, “Nilimuuliza Mtume (S.A.W); Ni kitendo gani ambacho Mungu anakipenda sana”, akasema “Ni swala kwa kipindi chake”. Nikauliza, “Kisha lipi”, akasema, “kuwatendea wazazi wawili mema”. Nikauliza tena, “kisha lipi”, akasema, “kujitolea katika njia ya Mungu”. (Bukhari na Muslim)
2. Imepokewa kutoka kwa Jabir (R.A.A) kuwa alisema, Mtume (S.A.W) amesema, “Mfano wa swala tano ni kama mto mkubwa unaopita mbele ya mlango wa mmoja wenu na ikawa mtu akaoga ndani ya mto huo kila siku mara tano”. (Muslim)
3. Imepokewa kutoka kwa Abu Thuraiyah Sabrah bin Ma‘bad Al-Juhani (R.A.A) kuwa alisema, Mtume (S.A.W) amesema, “Mfundisheni mtoto kuswali anapofika umri wa miaka saba na mchapeni anapofika miaka kumi akikataa kuswali” (au kuiacha). (Abu Dawud na Tirmidhi)
4. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.A) kuwa Mtume (S.A.W) amesema, “Swala tano (kikamilifu), na swala ya Ijumaa hadi Ijumaa, na saumu ya Ramadhani hadi Ramadhani huwa ni kafara ya madhambi yaliyo baina ya hivi vipindi, yanapotengwa mbali madhambi makubwa sana” (mfano wa kuua bila ya haki). (Muslim)
5. Imepokewa kutoka kwa Abul Yaqdhan Ammar Bin Yasir (R.A.A) kuwa alisema, “Nilimsikia Mtume (S.A.W) akisema, “Swala ndefu na hotuba fupi ya mtu ni alama ya ujuzi wake na fahamu njema, kwa hivyo refusheni swala na fupisheni hotuba”. (Muslim)