WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
SAUMU
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.A) kuwa alisema, Mtume (S.A.W) amesema, “Mtu ambaye hakuwacha kusema neno baya na kutenda jambo baya basi Mwenyezi Mungu hana haja kwa mtu huyo kuwacha chakula chake na kinywayi chake” (saum ina maana yakumtengeneza mtu wala si lengo kuwa kukaa na njaa na kiu tu). (Bukhari)
2. Imepokewa kutoka kwa Abu Ayub (R.A.A) kuwa alisema, Mtume (S.A.W) amesema, “Mtu aliyefunga mwezi wa Ramadhani na baada yake akafuatisha siku sita (6) za mwezi wa mfugo kwanza (Shawwal), basi mtu huyo ni kama aliyefunga mwaka mzima”. (Muslim)