WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
HIJJA
1. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (R.A.A) kuwa alisema Mtume (S.A.W) aliulizwa, ‘Kitendo gani ni bora zaidi?’ Mtume akajibu, “Ni kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake”. Akaulizwa, “Kisha ni kitendo gani bora zaidi?” Akajibu, “Nikujitolea kikamilifu katika njia ya Wenyezi Mungu”. Akaulizwa - “Kisha ni kitendo gani bora zaidi?” Akajibu, “Ni hijja isokuwa na kasoro”. (Bukhari na Muslim)
2. Imepokewa kutoka kwa Aisha (R.A.A), kuwa alisema nilimwambia Mtume (S.A.W), tunaonelea (sisi wanawake) kwamba jihadi (kujitolea kikamilifu kwa njia ya Mwenyezi Mungu hata kama ni kivita) ni tendo bora zaidi, “kwa hivyo kwanini hatuendi katika jihadi?” Mtume (S.A.W) alijibu, “lakini jihadi bora zaidi (kwenu nyinyi) ni hijja isokuwa na kasoro”. (Bukhari)