WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
IBADAH
Imepokewa kutoka kwa Bibi Aisha (ر ) kuwa alisema, “Alikuwa Mtume (ص ) zinapoingia siku kumi (za mwisho wa mwezi wa Ramadhani), Mtume (ص ) akikesha usiku kucha, na pia kuwaamsha watu wake wa nyumbani akifanya bidii pamoja na kuzidisha ibada”. (Bukhari na Muslim)- Imepokewa kutoka kwa Abu Musa Ash‘ari (ر ) kuwa alisema, Mtume (ص ) amesema, “Mmoja wa waja wa Mungu anapokuwa mgonjwa au anapo safiri huandikiwa kadiri ya yale aliyo kuwa akitenda alipokuwa mzima nyumbani”.(Bukhari)