Bismillah
 

WELCOME TO

 
Muhammad

MADRASA AL-HIDAYA

Allah
 

MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE

 

Al-Fatiha

Allah

Prophet Muhammad

Qur'an

Hadith

Home

What's New

Total Site Contents

Al-Fatiha

 

HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)

DUA

1.  Imepokewa kutoka kwa Abu Musa Ash‘ari (ر ) kuwa imepokewa kutoka kwa Mtume (ص ) kuwa alisema, “Hakika Mwenyezi Mungu hukunjua mkono wake usiku ili aliyetenda maovu mchana apate kutubu na hukunjua mkono wake mchana ili aliyetenda maovu usiku apate kutubu. Na ataendelea kufanya hivyo hadi jua litakapochomozea upande wa maghribi” (yaani siku ya kiyama). (Muslim)

2.  Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa alisema, nilimsikia Mtume (ص ) akisema, “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa mimi humuomba Mungu maghfira na kumrudia kwa toba mara sabini kila siku”. (Bukhari)

3.  Imepokewa kutoka kwa Abdallah Bin Masoud (ر ) kuwa Mtume (ص ) alikuwa akisema, “Ewe Mola nakuomba uongufu na uchaji (Mungu), na nitakase kutokana na yaliyoharamishwa; na (unipe) ukwasi”. (Muslim)                                           

4.  Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Hawakukaa watu katika kikao chochote wakakosa kumtaja Mungu aliyetukuka katika kikao hicho na vile vile wakawa watakosa kumswalia Mtume wao (ص ), isipokuwa watu hao watapata majuto. Basi Mungu akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe”. (Tirmidhi)

5.  Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas (ر ) kuwa alisema, “Nilimsikia Mtume (ص ) akisema, “Hakuna mtu yeyote muislamu afae kisha watu arobaini wasiomshirikisha Mungu kabisa wakisimama nyuma ya jeneza yake (kwa ajili ya kumswalia) ila Mwenyezi Mungu huikubalia shifaa yao kwa huyo maiti”. (Muslim)

 


 

 

 

 


HOME

DOOR 

WINDOWS