WELCOME TO |
||
MADRASA AL-HIDAYA |
||
MUSLIM SCHOOL OF RIGHT GUIDANCE |
HADITHI ZA MTUME MUHAMMAD
(Amani iwe juu yake)
WEPESI KATIKA DINI
- Imepokewa kutoka kwa Ibn Masoud (ر ) kuwa Mtume (ص ) amesema, “Wameangamia na kupotoka wenye kuweka mikazo zaidi katika ibada zao”. Na alisema hayo mara tatu. (Muslim)
- Imepokewa kutoka kwa Bi Aisha (ر ) kuwa alisema, “Mtume (ص) alikuwa akiacha kufanya jambo ingawaje apenda kulitenda, kwa hofu watu (waislamu) watalitenda kisha wakalifanya liwe faradhi juu yao”. (Bukhari na Muslim)
- Imepokewa kutoka kwa Bin Umar (ر ) kuwa alisema, “Tulikuwa tunapombai Mtume (ص) (kuapa juu ya utiifu) kwa kumsikiza na kumtii, alikuwa akituambia, “kwa kadiri mnavyoweza”. (Bukhari na Muslim)
- Impekewa kutoka kwa Anas Bin Malik (ر ) kuwa Mtume (ص ) alisema, “Yafanyeni mambo kuwa sahali na yanayowezekana na wala musiyafanye magumu. Muwabashirie watu (kuhusu mazuri yatakayotokea) na wala msiwafanye wawe na chuki”. (Bukhari na Muslim)